IQNA

Semina ya Kimataifa ya Qur'ani kufanyika Malaysia

12:23 - April 12, 2012
Habari ID: 2302936
Semina ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu katika Jamii ya Leo itafanyika Desemba Mosi na Pili mwaka huu katika Chuo Kikuu cha Zainul Abidin huko Terengganu nchini Malaysia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, semina hiyo imeandaliwa na Kitivo cha Masomo ya Kisasa ya Uislamu katika chuo hicho kwa ushirikiano na Taasisi ya Kimataifa ya Sayansi na Elimu za Kiislamu, serikali ya Jordan na serikali ya jimbo la Terengganu.
Warsha hiyo inatazamiwa kujadili masuala ya kisasa kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu na nafasi ya Qur'ani kama kitabu cha kipekee cha kubadilisha jamii kwa lengo la kufikia hali bora na saada.
Wanazuoni na watafiki walioalikwa kushiriki watawasilisha mada kama vile, Qur'ani Tukufu; Itikadi na Fikra, Qur'ani Tukufu; Fiqhi na Sheria, Qur'ani Tukufu; Sayansi na Teknolojia, Qur'ani Tukufu na Misaada kwa Jamii, Qur'ani Tukufu na Uchumi, Qur'ani Tukufu na Elimu, Tafsiri ya Qur'ani Tukufu na Ustawishaji Qur'ani Tukufu katika eneo la Terengganu.
Semina hiyo hufanyika kila baada ya miaka miwili.
983797
captcha