Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, usambazaji wa nakala hizo za Qur'ani umeanza Jumamosi alasiri 14 Aprili katika ukumbi wa Al Isala, imetangaza Idara ya Kutetea Qur'ani Jordan.
Aiman Riba ambaye ni mkurugenzi wa maendeleo katika wilaya ta Rasifa amehudhuria sherehe za kuzinduliwa nakala hizo za dijitali za Qur'ani Tukufu kwa lugha ya ishara.
Imedokezwa kuwa nakala hizo za Qur'ani ambazo zinawalenga walio na ulemavu wa masikio mbali na kuwa na aya kwa lugha ya ishara pia zina picha zinazofafanua maana ya aya.
Nakala hizo zilizo katika muundo wa CD zimetunukiwa wenye ulemavu wa masikio.
Lugha ya ishara ni lugha ambayo badala ya kutumia sauti, wazungumzaji wake hutumia ishara mbalimbali za mkono, vidole, mwili au uso kufikisha ujumbe.
984868