Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kikao hicho cha siku mbili kilichoanza leo Aprili 14 kimeandaliwa na Kituo cha Ahlul Bayt AS mjini Kinshasa.
Sheikh Issa Mubaki na Sheikh Daud Waneba ambao wote wamehitimu katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa nchini Iran na ambao ni wahadhiri katika vyuo vikuu na vyuo vya kidini watazungumza katika hafla hiyo.
Kikao hicho kitajadili hali ya Waislamu, hasa Mashia ambapo watajadili kuhusu hatari za kuenea itikadi za Kiwahabbi nchini Congo.
Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimi 10 ya watu milioni 70 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Uislamu uliingia nchini humo katika karne ya 18.
984626