Tovuti ya Leadership imeripoti kuwa Mkurugenzi wa Kamati ya Elimu za Kiislamu katika jimbo la Kebbi nchini Nigeria Alhaji Minasara Sajo ametangaza kuwa bajeti hiyo imetengwa kwa ajili ya kustawisha elimu na taaluma za Kiislamu.
Ameongeza kuwa kutokana na bajeti hiyo pia sasa mashindano ya Qur'ani Tukufu yatakuwa yakifanyika kwa mpangilio maalumu katika jimbo hilo.
Mkurugenzi wa Kamati ya Elimu za Kiislamu wa jimbo la Kebbi ameashiria mafanikio ya jimbo hilo katika uwanja wa kusimamia mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani Tukufu na kusema kuwa sehemu ya bajeti hiyo itatumiwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mbinu za kiraa na hifdhi ya Qur'ani. 985175