Nakala biyo iliandikwa katika kipindi cha utawala wa Watatari.
Televisheni ya Press imeripoti kuwa, nakala hiyo ya aina yake ya Qur'ani Tukufu ina upana wa sentimita 2 kwa tatu na inahifadhiwa katika kisanduku cha fedha.
Mkusanya vitabu wa Ukraine anayehifadhi nakala hiyo ya Qur'ani anasema ina umri wa miaka 200 na kwamba ina thamani kubwa katika upande wa masuala ya sanaa.
Nchi ya Ukraine ambayo ni kiunganishi cha ustaarabu na tamaduni mbalimbali za Mashariki na Magharibi, ina athari nyingi za kale na adimu mno za vitabu vya Kiislamu.
Maktaba za nchi hiyo zinasifika kwa kuwa na nakala nyingi na za aina mbalimbali za Qur'ani na vitabu vingi vilivyoandikwa katika karne zilizopita. 984974