IQNA

Misahafu laki moja yasambazwa Ethiopia

22:50 - April 15, 2012
Habari ID: 2305016
Jumuiya ya Uturuki ya Kutoa Misaada ya Kibinadamu IHH (Insani Yardim Vakfi ) imeanza mpango maalumu wa kusambaza nakala laki moja za Qur'ani Tukufu nchini Ethiopia.
Kwa mujibu wa tovuti ya e-haberajansi, Jumuiya ya Uturuki ya Kutoa Misaada ya Kibinadamu ikishirikiana na Jumuiya ya Misaada ya Anatolia imeanza kutekeleza mpango wa kusambaza Misahafu lakini moja katika misikti na vituo vya Kiislamu kote Ethiopia.
Taarifa ya Jumuiya ya Uturuki ya Kutoa Misaada ya Kibinadamu ameashiria uhaba wa Misahafu nchini Ethiopia na kusema baadhi ya Waislamu wanaotaka kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini humo, kutokana na uhaba wa Misahafu' huhifadhi na kusoma sura au aya kadhaa na kisha huwaazima wenzao Msahafu kama amana ili nao waweze kunufaika na wakati mwingine hukaa hata siku 20 bila Msahafu na hili hufanya zoezi la kuhifadhi Qur'ani kuwa gumu sana.
Hivi karibuni timu ya IHH ilitembelea Ethiopia, ambayo ni kati ya nchi masikini zaidi za Afrika, na kusambaza nakala 13,000 za Qur'ani.
Waislamu nchini Ethiopia na maeneo mengine ya Afrika hulipa umuhimu sana suala ya mafunzo ya Kiislamu hasa ya Qur'ani ili kukabiliana na njama za Wamishonari wa Kikristo barani humo.
Inakadiriwa kuwa kati ya watu takribani milioni 82 Ethiopia, milioni 55 ni Waislamu.
985856
captcha