IQNA

Al Azhar yaandaa semina za Miujiza ya Qur'ani

17:50 - April 16, 2012
Habari ID: 2305952
Chuo Kikuu cha Al Azhar mjini Cairo Misri kinaandaa mfululizo wa semina kuhusu miujiza ya Qur'ani Tukufu.
Semina hizo zimeandaliwa kama sehemu ya programu za Wiki ya Sayansi ya Al Azhar ambayo ilianza Aprili 14 katika kitivo cha sayansi chuoni hapo na kuendelea hadi Aprili 16.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Balad kati ya semina zitakazofanyika wiki hii ni pamoja na 'Lugha ya Sayansi na Nambari' na 'Nafasi ya Seli Shina katika Ustawi wa Sayansi za Tiba'.
Kamati ya kisayansi imeteuliwa kuratibu semina hizo na kati ya wanachama wake ni Osama al Abd, Mohammad Hassan Ivaz na Hassan Siraj.
Chuo Kikuu cha Al-Azhar ambacho kilipewa jina hilo kwa heshima ya Fatima Zahra (AS) binti ya Mtume Muhammad (SAW) katika Cairo ni chuo kinachoheshimiwa kati ya Waislamu duniani kama kitovu cha elimu ya kidini. Baada ya chuo cha Al-Qairawan mjini Fez (Morocco) ni chuo kikuu cha kale duniani kinachoendelea hadi leo hii.
Al-Azhar imejulikana hasa kama chuo cha Kiislamu lakini leo hii kuna idara nyingi kama vile madhab, lugha ya Kiarabu, tiba, ualimu, uhandisi na nyengine.
986656
captcha