Akizungumza na IQNA, Mohammad Hussein Ayati anayesimamia masuala ya utamaduni katika wizara hiyo, amesema kuwa lengo kuu la kitengo hicho ni kustawisha utafiti wa masuala ya tiba na Qur'ani.
Huku akiashiria semina kadhaa zilizoandaliwa na wizara hiyo kuhusu Qur'ani na Tiba, Ayati amesema, 'tutafanya juhudi za kuhakikisha kuwa mipango wa Wizara ya Afya inaenda sambamba na mafundisho ya Qur'ani Tukufu'.
Amesema kitengo maalumu cha Qur'ani katika Wizara ya Afya kitaandaa vikao vya kila wiki kuhusu masuala ya Qur'ani.
Aidha ameashiria kongamano la kitaifa la Qur'ani na Tiba litakalofanyika Mei mjini Tehran na kuongeza kuwa kikao hicho kinapanga kuangazia suala la mbinu za utafiti katika utafiti wa Qur'ani.
985375