IQNA

Kongamano la kimataifa la Ustawi wa Utafiti wa Masuala ya Qur’ani kufanyika Saudia

23:59 - April 16, 2012
Habari ID: 2306315
Kongamano la kimataifa la Ustawi wa Utafiti wa Masuala ya Qur’ani litafanyika mapema mwaka ujao katika Chuo Kikuu cha Mfalme Saud nchini Saudi Arabia.
Gazeti la al Sharq linalochapishwa nchini Saudi Arabia limeripoti kuwa utangulizi wa mkutano huo unafanywa na kitengo cha sayansi ya Qur’ani cha Chuo Kikuu cha Mfalme Saud na Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Qur’ani cha Saudia.
Msimamizi wa Kitengo cha Sayansi ya Qur’ami katika Chuo Kikuu cha Mfalme Saud Bwana Abdurahman al Shahri amesema kuwa ajenda kuu za kongamano hilo ni pamoja na uhakiki mbalimbali kuhusu masuala ya Qur’ani na njia kustawisha uhakiki huo katika nyanja mbalimbali za sayansi ya Qur’an ikiwemo tafsiri, kiraa na kadhalika.
Amesema kuwa ajenda nyingine za kongamano hilo ni kuchunguza njia za kuhamasisha utafiti zaidi wa masuala ya Qur’ani, kutenga zawadi kwa watafiti bora, uwekezaji katika tasnifu zinazojadili masuala ya Qur’ani na kuimarisha utamaduni wa wakfu kwa mujibu wa mtazamo wa Qur’ani.
Al Shahri ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Mfalme Saudi pia kitachunguza njia za kutumia vyombo vya mawasiliano ya umma kwa ajili ya kuhudumia Qur’ani Tukufu na sayansi ya Qur’ani na vilevile njia za kuimarisha uhusiano kati ya vyombo vya mawasiliano ya umma na taasisi zinazojishughulisha na masuala ya Qur’ani. 987010

captcha