Kwa mujibu wa gazeti la Al Sharq , kongamano hilo litasimamiwa na Chuo Kikuu cha Mfalme Saudi kwa ushirikiano na Taasisi ya Tafseer al Qur'an.
Katibu wa kongamano hilo Abdul Rahman al Shahri amesema katika taarifa kuwa tarjuma, qiraa, tajweed na masomo ya kisasa ya Qur'ani ni kati ya mada muhimu zitakazojadiliwa katika kongamano hilo.
Amesema masuala mengine yatakayo jadiliwa ni uratibu wa masuala ya utafiti wa Qur'ani kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi za Qur'ani na vyombo vya habari na kutumia teknolojia ya kisasa katika utafiti wa Qur'ani.
987010