Gazeti la al Rai la Kuwait limeripoti kuwa siku ya tano ya mashindano ya Qur'ani Tuzo ya Kuwait imetawaliwa na mchuano mkali baina ya wasomaji kutoka bara Afrika katika nchi kama Nigeria, Tanzania, Sierra Leone, Ivory Coast, Gambia, Djibouti, Comoro na Somalia.
Nchi 46 za Kiislamu na 4 zisizo za Kiislamu ambazo ni Russia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bosnia na Serbia pia zinashiriki katika mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Qur’ani ya Kuwait Khalid Bugheit amesema kuwa mashindano hayo yanafanyika katika vitengo vinne vya hifdhi ya Qur’ani nzima pamoja na tajwidi, kiraa saba, kiraa na tajwidi ya Qur’ani na teknolojia bora zidi ya kuhudumia Qur’ani Tukufu.
Wasomaji Muhammad Javad Muhammadi na Redha Golshahi kutoka Iran wanashiriki katika mashindano hayo.
Mashindano hayo ya kimataifa yatamaliza shughuli zake kesho na washindi wa kwanza wa mashindano hayo watatunukiwa zawadi ya dinari laki moja na elfu 14 za Kuwait.987868