IQNA

Mkristo anamiliki nakala ndogo zaidi ya Qur'ani Imarati

21:39 - April 17, 2012
Habari ID: 2307106
Mkristo mmoja anayeishi katika Umoja wa Falme za Kiarabu anamiliki nakala ndogo zaidi ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani iliyoandikwa kwa hati za mkono.
Tovuti ya emaratalyoum imeripoti kuwa nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu ina umri wa miaka 300 na kurasa zake zina urefu wa sentimita 1.5 na upana wa sentimita 0.8.
Nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu si kamili ya kitabu hicho na idadi kadhaa ya nakala zake imetoweka.
Mkristo huo raia wa Jordan anayeishi Imarati ambaye anahifadhi nakala hiyo ya Qur'ani anasema nakala hiyo ilipatikana katika eneo lililo karibu na Msikiti wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kwamba yeye mwenyewe amerithi Qur'ani hiyo kutoka kwa babu yake mzaa baba.
Amesema kuwa mwaka 1998 aliwaandikia barua viongozi wa Shirika la Uchapishaji Qur'ani la Mfalme Fahad nchini Saudi Arabia na kuwapasha habari ya nakala hiyo ya Qur'ani. Ameongeza kuwa wakati huo walitoa pendekezo la kununua nakala hiyo kwa riale milioni 3 za Saudia lakini alikataa kwa sababu hataki kupoteza nakala hiyo ya Qur'ani. 987659


captcha