IQNA

Kijana Muirani ashika nafasi ya tatu mashindano ya Qur'ani ya Kuwait

21:54 - April 18, 2012
Habari ID: 2307900
Karii kijana wa Iran Ridha Golshahi ameshika nafasi ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaliyomalizika jana nchini Kuwait.
Afisa anayeshughulikia masuala ya habari katika Ofisi ya Utamaduni ya Iran nchini Kuwait Shahram Salamati amesema kuwa katika kila kitengo cha mashindano hayo waliteuliwa wasomaji bora 5 na kwamba Ridha Golshahi ameshika nafasi ya tatu katika kiraa ya Qur'ani Tukufu.
Salamati amesema kuwa Ridha Golshahi mwenye umri wa miaka 14 ameng'ara sana kati ya wasomaji 140 wa Qur'ani kutoka nchi 70 duniani.
Karii kutoka Morocco ameshika nafasi ya kwanza ya mashindano ya kiraa ya Qur'ani. Katika upande wa hifdhi ya Qur'ani wasomaji kutoka Misri, Niger, Saudi Arabia, Libya na Kuwait walishika nafasi ya kwanza hadi tano.
Washindi wa kwanza wa mashindano hayo wametunukiwa zawadi ya dinari laki moja na elfu 14 za Kuwait.
Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Qur’ani ya Kuwait Khalid Bugheit amesema kuwa mashindano hayo yamefanyika katika vitengo vinne vya hifdhi ya Qur’ani nzima pamoja na tajwidi, kiraa saba, kiraa na tajwidi ya Qur’ani na teknolojia bora zidi ya kuhudumia Qur’ani Tukufu. 988885


captcha