IQNA

Wanafunzi wa Russia wachuana katika mashindano ya kiraa ya Qur'ani

21:54 - April 18, 2012
Habari ID: 2307901
Mashindano ya kiraa ya Qur'ani na hifdhi ya hadithi za Mtume Muhammad (saw) makhsusi kwa wanafunzi wa kike wa shule za Kiislamu yalimalizika juzi katika jimbo la Nizhny Novgorod huko Russia.
Mashindano hayo yalifunguliwa kwa kisomo cha Qur'ani na hotuba ya Ghiyadh Hadhrat Zakirov ambaye ni Mwenyekiti wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu wa jimbo la Nizhny Novgorod ambaye aliashiria umuhimu wa elimu na maarifa na kusema kuwa mtafutaji wa elimu na maarifa ya Uislamu huwa kigezo bora katika jamii na umma wa Kiislamu.
Sambamba na mashindano hayo kulikuwepo pia mashindano ya maarifa na sayansi ya Qur'ani na washindi wa mashindano hayo walitunukiwa zawadi.
Katika upande wa mashindano ya hadithi za Mtume (saw) kundi la Madrasa ya Arafat limeibuka na ushindi. 988531

captcha