Gazeti la Gardian limeandika kuwa yapata mwaka mmoja uliopita kasisi huyo wa Marekani alichoma moto nakala za Qur'ani Tukufu, suala ambalo lilisababisha mapiganoi makali mbele ya makao ya Umoja wa Mataifa mjini Mazar Sharif huko Afghanistan na kuuawa maafisa 7 wa taasisi hiyo ya kimataifa. Kitendo hicho kiovu pia kilizusha malalamiko ya Waislamu kote duniani.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Bill Speaks amesema kuwa Washington inaelewa vyema vitishi vilivyotolewa na Kasisi Jones vya kuchomwa moto Qur'ani na inafuatilia kwa makini hali ya mambo.
Wakati huo huo Mwakilishi wa Kabul katika Bunge la Afghamistan Sayed Hussani Balkhi amesema kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu ni kitendo kiovu ambacho kinapaswa kulaaniwa na jamii ya kimataifa.
Vilevile Jamshid Hashimi ambaye ni mdhadhiri wa mojawapo ya vyuo vikuu vya Afghanistan amesema Uislamu hauwaruhusu wafuasi wake kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Wakristo, kwa msingi huo Wakristo pia wanalazimika kuheshima kitabu kitukufu cha Waislamu. 990469