IQNA

OIC yaandaa kongamano la 'Wakimbizi katika Ulimwengu wa Kiislamu'

16:41 - April 23, 2012
Habari ID: 2310709
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imepanga kongamano la siku mbili la mawaziri kuhusu 'Wakimbizi Katika Ulimwengu wa Kiislamu' kwa ushirikiano na Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR huko Ashgabat, Turkmenistan , kuanzia Mei 10.
Katika taarifa, OIC imesema kongamano hilo linalenga kuashiria nafasi ya OIC na nchi wanachama katika kuwasaidia wakimbizi pamoja na jukumu la UNHCR kuhusu wakimbizi.
Kongamano hilo pia linalenga kuimarisha ufahamu kuhusu tatizo la wakimbizi katika nchi wanachama wa OIC pamoja tatizo la wakimbizi duniani.
Imedokezwa kuwa nchi za Kiislamu zina asilimia 52 ya watu wanaohudumiwa na UNHCR wakiwemo wakimbizi wa nje na ndani ya nchi, wanaotafuta hifadhi ya kisiasa, wanaorejea makwao na watu wasio na utaifa. Idadi hii haijumuishi wakimbizi Wapalestina ambao wanahudumiwa na kitengo maalumu cha Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa UNHCR hadi mwaka 2010 kulikuwa na takribani wakimbizi Milioni 17.76 katika ulimwengu wa Kiislamu ambapo Iran na Pakistan zimewapa hifadhi zaidi ya asilimia 30 ya wakimbizi wote duniani.
991685
captcha