Tovuti ya sabr.cc imeripoti kuwa baada ya kuingia katika chumba cha mfanyakazi mmoja wa mahakama hiyo, mkaguzi huyo wa serikali ya Algeria alipekua vifaa binafsi vya mfanyakazi huyo na kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa kuirusha chini.
Afisa huyo ambaye alikuta kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika maktaba ya mfanyakazi huyo wa mahakama ya Algiers alimdhalilisha na kumuuliza kwa nini alikuwa ameweka Qur'ani mahala hapo kisha akatupa chini nakala hiyo ya Qur'ani.
Baada ya tukio hilo mfanyakazi ambaye alikuwa meweka nakala hiyo ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika maktaba yake aliwasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya afisa huyo.
Wafanyakazi waliokuwepo hapo walisema kuwa wanaheshimu sheria inayowazuia kusoma Qur'ani wakati wa kazi.
Watu walioshuhidia kitendo hicho kiovu wamesisitiza kuwa hatua hiyo ya afis wa serikali ilikuwa kinyume cha sheria na kwamba kukivunjia heshima kitabu kitukufu cha Qur'ani ni kosa kubwa. 991871