Tovuti ya egynews imeripoti kuwa, Kasisi Scott Morgan wa Marekani amefunza aya za Qur’ani katika kanisa hilo ambazo zinazungumzia masuala ya mwanamke, kuishi kwa amani na haki za raia na kueleza maana ya aya hizo kwa hadhirina.
Kasisi Scott Morgan amesisitiza kuwa amechagua maudhui ya mwanamke na ukatili ambazo ni muhimu kwa Wamarekani na kufundisha aya za Qur’ani zinazozungumzia masuala hayo kwa kueleza kuwa Uislamu ni dini inayokataza ukatili dhidi ya wasiokuwa Waislamu, na kwamba katika suala hilo ametegemea sira na mwenendo wa Mtume Muhammad (saw).
Kasisi Morgan ameongeza kuwa, amebainisha na kueleza pia nafasi ya mwanamke katika Uislamu na mchango wake katika jamii kwa mujibu wa aya za Qur’ani.
Kanali moja ya televisheni ya Marekani imerikodi na kurusha hewani vikao vya darsa za Kasisi Morgan na kuripoti kuwa: “Wakati katika jimbo la Florida kuna watu kama Kasisi Terry Jones ambao anachoma moto nakala za kitabu cha Qur’ani, katika jimbo la Virginia kuna Scott Morgan ambaye anafundisha Qur’ani kanisani.”
Kanali hiyo ya televisheni ya Marekani imeripoti kuwa, Kasisi Scott Morgan alijuana na Waislamu na Uislamu akiwa bado mdogo na katika kipindi cha mwishoni mwa muongo wa 1970 aliishi katika jamii ya Waislamu wa Afghanistan na kujifunza misingi na thamani za Kiislamu. 994669