Tovuti ya ctme.co.za imeripoti kuwa, semina hiyo inasimamiwa na Academia ya Sayansi za Kiislamu ya Afrika Kusini kwa shabaha ya kuwaelimisha zaidi Waislamu kuhusu elimu ya tafsiri ya Qur’ani na kutayarisha uwanja mzuri wa watu kuelekea kwa Mola Muumba.
Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa katika semina hiyo ni pamoja na maendeleo ya elimu ya tafsiri ya Qur’ani, aina za tafsiri za Qur’ani, tafsiri mashuhuri za Qur’ani, maudhui za Qur’ani Tukufu, tafsiri ya Suratu Maryam, tafsiri na usasa, uchunguzi kuhusu tarjumi za Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiingereza, misingi ya kutafakari katika Qur’ani Tukufu na kadhalika.
Maulama na watafiti 6 wa masuala ya tafsiri ya Qur’ani wanazungumzia masuala mbalimbali katika semina hiyo. 994622