IQNA

Kongamano la Imam Khomeini kufanyika mwaka 2012 mjini London

17:09 - April 29, 2012
Habari ID: 2314307
Kongamano kuhusu shakhsia ya Imam Ruhullah Khomeini litafanyika London kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Ahlul Bayt (AIM) na Kituo cha Kiislamu cha England.
Kongamano hilo litakalofanyikwa kwa anwani ya 'Tafakari Kuhusu Uongozi' litafanyika katika Kituo cha Kiislamu England katika mji wa London Juni 3, 2012.
Wazungumzaji waalikwa katika kongamano hilo ni pamoja na Sheikh Moezi, Sheikh M. Saeed Bahmanpour, Kasisi Frank Julian Gelli, Nabil Ahmed Awan, na Sheikh Hamza Sodagar. Watu kutoka matabaka mbalimbali ya jamii wako huru kuhudhuria kongamano hilo.
Washiriki watajadili masuala kama vile mfumo wa utawala au uongozi, uhusiano wa wafuasi wa dini mbalimbali, kufuata mafunzo ya Watu wa Nyumba ya Mtume SAW (Ahlul Bayt), hali ya vijana pamoja na hali ya Waislamu katika mataifa mbalimbali.
995430
captcha