Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Oman ONA, mashindano hayo ya kitaifa ambayo ni ya 22 yalianza jana usiku ambapo zaidi ya mahafidh 15 wa Qur'ani wanachuana katika Msikiti Mkuu wa Sultan Qaboos katika eneo la Nizwa Katika mkoa wa ad- Dakhiliyah.
Mahafidh hao ni kati ya mahafidh 142 walioshiriki katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo mikoani ambapo walishinda na kupata fursa ya kushiriki katika hatua ya nusu fainali.
Baada ya mahafidh hao kuchuana katika hatua hii watakaofanikiwa kushinda watachaguliwa ili kushiriki katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo ambayo imepangwa kufanyika tarehe 9 Mei.
Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Sultan Qaboos. 995476