IQNA

Kitabu cha 'Utafiti katika Historia ya Qur'ani Tukufu' chashinda Russia

17:45 - April 30, 2012
Habari ID: 2315402
Kitabu cha 'Utafiti katika Historia ya Qur'ani Tukufu' ambacho kimeandikwa na Sayyid Muhammad Baqir Hujjati ni miongoni mwa vitabu vinne bora vilivyoshinda katika maonyesho ya vitabu vilivyoandikwa mwaka 2011 katika kitengo cha fasihi ya kimaanawi na historia ya kidini huko Russia.
Kitabu hicho kiliarifishwa katika maonyesho hayo yaliyomalizika hivi karibuni huko St. Petersburg nchini Russia na Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu kwa ushirikiano wa Idara ya Mamufti wa Russia. Kitabu hicho kinachozungumzia mafundisho ya Qur'ani Tukufu, kimewavutia wasomi wengi tokea kilipochapishwa.
Maonyesho hayo ya 21 yameyashirikisha mashirika 167 kutoka majimbo 37 ya Russia. 996482
captcha