Huku ikisisitiza nafasi muhimu ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC katika matukio ya Afghanistan, serikali ya Uturuki imetaka Ekmeleddin Ihsanouglu, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo ashirikishwe katika kikao kijacho cha shirika la kujihami la nchi za Magharibi Nato.
Siku chache zilizopita serikali ya Uturuki ilipinga vikali kushirikishwa kwa watawala wa Israel katika kikao kijacho cha Nato ambacho kimepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Mei huko Chicago Marekani na kushurutisha kushiriki kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya katika kikao hicho na kushirikishwa Katibu Mkuu wa OIC katika kikao hicho.
Akizungumzia suala hilo hivi karibuni afisa mmoja wa ngazi za juu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki amesema OIC imekuwa na nafasi muhimu katika kushughulikia masuala ya Afghanistan na kusema kuwa serikali ya Ankara imeshurutisha kushiriki viongozi wa Umoja wa Ulaya katika kikao hicho na kushirikishwa pia Katibu Mkuu wa OIC, lakini akaongeza kwamba hadi sasa haijapata jibu kutoka kwa wahusika kuhusiana na suala hilo. 996748