Taarifa ya Sheikh Muhammad Hussein imelaani kitendo hicho kiovu na kusema kuwa kinapingana na mafundisho ya dini zote za mbinguni na thamani za kimaadili.
Ameongeza kuwa hatua kama hizo zinachochea zaidi moto wa fitina na chuki za kidini.
Mufti wa Palestina ametahadharisha juu ya kuendelezwa vitendo kama hivyo viovu na kusema kuwa vinachochea ghasia na machafuko kati ya wafuasi wa dini mbalimbali.
Vilevile amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya maovu hayo ya kasisi wa Marekani dhidi ya dini tukufu ya Uislamu na Waislamu na amewataka watetezi wa amani kote duniani kufanya juhudi za kuzuia vitendo kama hivyo.
Kasisi Terry Jones wa Marekani Jumamosi iliyopita alichoma moto nakala ya kitabu kitukufu cha Qur'ani mbele ya wapiga picha na kusambaza picha hizo katika mtandao wa intaneti. 996888