IQNA

Mashidano ya Qur'ani Qatar yaanza

12:32 - May 01, 2012
Habari ID: 2315469
Mashidano ya 19 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Qatar yameanza katika mji mkuu wa Qatar, Doha. Kwa mujibu wa gazeti la Ash Sharq, raia 1500 wa Qatar pamoja na wafanyakazi wa kigeni watashiriki katika vitengo vyote vya kuhifadhi Qur'ani katika mashindano hayo.
Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kuwahimiza watu kuhifadhi na kutafakari katika aya za Qur'ani Tukufu na kuwashajiisha vijana kujikurubisha na Qur'ani Tukufu.
Jopo la majaji linaongozwa na Sheikh Ahmad Al Misrawi qarii mtajika wa Misri na Mohammad al Mahmoud ambaye ni mkuu wa kamati inayoandaa mashindano.
Washindi watapata zawadi za Riali za Qatar 36,000 hadi 60,000.
Maonyesho ya Qur'ani pia yatafanyika pembizoni mwa mashindano hayo.
996561
captcha