IQNA

Iran yalaani uvunjiwahi heshima Qur'ani huko Marekani

12:42 - May 01, 2012
Habari ID: 2315640
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hatua ya Kasisi Terry Jones wa Kanisa la Dove World Outreach Center katika mji wa Gainsville jimboni Florida Marekani kurudia tena kitendo kichafu cha kuichoma moto Qur'ani Tukufu.
Taarifa ya Waizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kitendo kama hicho ni sehemu ya njama zilizofeli za nchi za Magharibi za kuanzisha vita vya staarabu. Taarifa hiyo imesema kitendo hicho kinalenga kuchochea chuki dhidi ya Uislamu. Iran imelaani pia serikali ya Marekani kwa kushindwa kuzuia kitendo hicho za chuki dhidi ya Uislamu.
Wakati huo huo mbunge mmoja wa Iran amesema utawala wa Saudi Arabia ni mshirika katika kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani huko Marekani kutokana na kimya chake baada ya kitendo hicho kichafu.
Mohammad Esmail Kowsari amesema, 'Watawala wa Saudi Arabia wanadai kuwa ni walinzi wa Al Ka'aba na Msikiti wa Mtume SAW huko Madina (Haramain) lakini si tu kuwa wamenyamaza kimya baada ya Qur'ani kuchomwa moto na Wamarekani bali pia ni waitifaki wa Marekani.'
Hii ni mara ya pili kwa kasisi huyo mwovu kuchukua hatua kama hiyo ya kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Waislamu.
Mwaka uliopita Kasisi Terry Jones alitishia kuchoma moto Qur'ani Tukufu katika makumbusho ya matukio ya kigaidi ya Septemba 11 nchini Marekani lakini alilazimika kutotekeleza tishio hilo kutokana na mashinikizo ya kimataifa.
996334
captcha