IQNA

Kituo cha kuhifadhi nuskha za Qur'ani zilizoandikwa kwa mkono kuasisiwa Imarati

17:03 - May 02, 2012
Habari ID: 2316313
Kamati inayoandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tuzo ya Dubai imetangaza habari ya kuasisiwa hivi karibuni kituo cha nuskha za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa mkono huko Imarati, kitakachojulikana kwa jina la Sheikh Muhammad bin Rashid.
Kamati hiyo imesema kituo hicho kitaasisiwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo katika majengo ya makao makuu mpya ya Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu Tuzo ya Dubai.
Akizungumzia suala hilo, Ibrahim Muhammad Bumulihha mkuu wa kamati hiyo amesema kituo hicho kitakuwa kikikusanya na kuhifadhi nuskha za kale zilizoandikwa kwa mkono na vitabu vingine vinavyohusiana na Qur'ani pamoja na hadithi za Mtume Muhammad (saw).
Amesema vitabu hivyo vitakuwa vikihifadhiwa au ikilazimu, kukarabatiwa katika kituo hicho kwa kutumiwa teknolojia ya kisasa kabisa.
Ameongeza kuwa tayari Sheikh Muhammad bin Rashid Aal Maktum, mtawala wa Dubai ametoa nuskha zake binafsi za Qur'ani zilizoandikwa kwa mkono na kuzikabidhi kwa ajili ya kuhifadhiwa katika kituo hicho. 997548
captcha