Gazeti la al Youm al Sabi limeandika kuwa chombo cha kuaminika ndani ya Wizara ya Wakfu ya Misri kimeripoti kuwa nakala hiyo ya Qur'ani ambayo ilikuwa ikihifadhiwa katika Wizara ya Wakfu imeibwa na kundi la watu wasiojulikana.
Chombo hicho kimeongeza kuwa baada ya kuvunja uzio wa kuingia katika jengo la wizara hiyo, kundi hilo limeingia ndani na kuiba nakala hiyo ya Qur'ani.
Kimesema kuwa nakala hiyo ya Qur'ani si ya kihistoria na ni chapa ya kawaida.
Polisi imeaanza uchunguzi kuhusu tukio hilo la kuibwa nakala ya Qur'ani ya Wizara ya Wakfu.
Nakala hiyo ya Qur'ani inarejea katika zama za rais wa zamani wa Misri Gamal Abdel Naseer. Wizara ya Wakfu ya Misri ilimtunuku kiongozi huyo nakala hiyo ya Qur'ani baada ya mapinduzi ya mwaka 1952 na ilirejeshwa tena kwenye wizara hiyo baada ya kufariki dunia Abdel Nasser. 1000248