IQNA

Chama cha Mwafaka wa Kitaifa Lebanon chalaani kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani huko Marekani

11:26 - May 06, 2012
Habari ID: 2319290
Chama cha mwafaka wa Kitaifa nchini Lebanon kimeleni vikali kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Gazeti la al Intiqad linalochapishwa nchini Lebanon limeandika kuwa Mwenyekiti wa chama cha mwafaka wa Kitaifa cha Lebanon Bilal Taqiyuddin amesema kuwa hatua hiyo ya dharau na isiyofaa ya Kasisi Terry Jones wqa Marekani imeweka wazi kinyongo na uhasama wake na inatekelezwa katika fremu ya mipango maalumu ya kuzusha hitilafu na mgawanyiko kati ya Ulimwengu wa Kiislamu na Kikristo.
Ameongeza kuwa viongozi wa Marekani ambao daima wamekuwa wakizungumzia suala la kuheshimu haki za binadamu, thamani na matukufu ya kidini, wanapaswa kuzuia wimbi hilo la kuhujumu matukufu ya Kiislamu.
Bilal Taqiyuddin amesema kuwa mienendo kama hiyo imekuwa ikikaririwa mara kwa mara na katika vipindi tofauti kwa shabaha ya kuzusha ugomvi na mivutano kati ya Waislamu na Wakristo na kuhoji kuwa je, harakati hizi zimelaaniwa na Wakristo kama walivyofanya Waislamu? Je, harakati hizi hazipingani na mafundisho ya Ukristo? 1000524

captcha