IQNA

Mashindano ya tatu ya Qur'ani kufanyika Canada

11:24 - May 06, 2012
Habari ID: 2319295
Mashindano ya tatu ya kiraa na hifdhi ya Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 3 Juni nchini Canada yakisimamiwa na Ofisi ya Kituo cha Kiislamu cha kaskazini mwa nchi hiyo.
Mashindano hayo ambayo ni makhsusi kwa ajili ya watoto na mabarobaro yatafanyika kwa lengo la kuhamasisha kizazi kipya kusoma Qur'ani Tukufu
Katika upande wa wavulana, washiriki wenye umri wa kati ya miaka 12 na 17 watachuana katika hifdhi ya sura ya Qamar, hifdhi ya sura ya Buruj kwa wale wenye umri wa kati ya miaka 8 na 11, hifdhi ya sura ya Adiyat kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 na 7 na kiraa ya sura ya Israa kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 8 hadi 12.
Wasichana wenye umri wa miaka 8 hadi 11 pia watashindana katika hifdhi ya sura ya Buruj, miaka 5 hadi 7 hifdhi ya suratul Adiyat na kiraa ya suratu Israa kwa wasichana wenye umri wa miaka 8 hadi 12.
Washindi wa mahindano hayo watatunukiwa zawadi nono. 1000588
captcha