Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sensa hiyo ambayo imefanywa na Jumuiya ya Wanatakwimu wa Bodi za Kidini Marekani yenye makao yake Chicago, idadi ya Waislamu Marekani imeongezeka takribani maradufu muongo moja uliopita.
Inakadiriwa kuwa idadi ya Waislamu Marekani hadi mwaka 2010 ilikuwa ni milioni 2.6 kutoka milioni moja mwaka 2001.
Takwimu zisizo rasmi zinasema idadi ya Waislamu nchini Marekani ni kati ya milioni sita hadi milioni saba.
Sensa hiyo imeonyesha kuwa Waislamu sasa wanawazidi Mayahudi maeneo ya kati-magharibi na kusini mwa Marekani.
Ripoti zinasema ongezeko la idadi ya Waislamu huko Marekani ni kutokana na watu kusilimu na uhamiaji.
Uchunguzi huo ulionyesha kuwa kuna zaidi ya misikiti 2,000 kote Marekani ambapo 166 iko Texas.
Ripoti nyingine ya hivi karibuni ilionyesha kuwa idadi ya misikiti Marekani pia iliongezeka maradufu katika muongo mmoja uliopita na kufikia 2,000.
Uislamu unastawi kwa kasi Marekani pamoja na kuwepo wimbi kubwa la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
1000636