Akizungumza na mwandishi wa IQNA mjini Tehran pembizoni mwa kongamano lenye anwani ya: "Dini na Mwamko wa Zama Hizi", Stalin Gereselassie ameongeza kuwa dini ni chimbuko la utawala bora, haki za binadamu na demokrasia.
Akiashiria harakati za mwamko wa Kiislamu, amesema harakati hizi zimejengeka katika misingi ya kidini.
Amesema mwamko wa Kiislamu katika nchi za Kiarabu umewawezesha wananchi kufahamu kwa kina utendaji kazi wa serikali.
Kwa mujibu wa Gebresellasie, mwamko huu haujaishia tu katika nchi za Kiarabu bali sasa unashuhudiwa katika nchi mbalimbali za dunia kama vile Marekani kupitia 'Harakati ya Kukalia Wall Street'. Amesema harakati hii iliibuka baada ya Mwamko wa Kiislamu Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.
Ametabiri kuwa katika siku za usoni harakati hizi zinaweza kufikia malengo kama vile haki za binadamu.
Mtaalamu huyo wa mawasiliano wa Ethiopia amesisitiza kuwa mwamko wa Kiislamu utasababisha mabadiliko makubwa katika nchi za Kiarabu na madola ya kibeberu duniani.
1000617