Kati ya mada zitakazojadiliwa katika mihadhara hiyo ni Wahyi na mafundisho ya Qur'ani Tukufu. Aidha suala la qiraa ya Qur'ani pia litajadiliwa na wasomi.
Mada zingine zitakajojadiliwa ni kuhusu hitajio la Wahyi, namna Mtume SAW alivyopokea Wahyi, yaliyojiri katika Wahyi wa kwanza, itikadi potofu za Mustashrikin, namna Malaika Jibril alivyomletea Mtume SAW Wahyi na ufunuo, kujifunza na kusomesha Qur'ani Tukufu, Maisha ya Mtume SAW huko Makka na Madina, namna ya kuhifadhi Qur'ani, nafasi ya Masahaba katika kukusanya Qur'ani, historia ya Qur'ani Tukufu Afrika Kusini, jukumu la Waislamu kuhusu Qur'ani na kutekeleza Qur'ani katika maisha yetu.
1002230