IQNA

Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani kufanyika Ufaransa

15:09 - May 07, 2012
Habari ID: 2320514
Mashindano ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika tarehe 15 na 16 Septemba katika mji wa Val d'Oise nchini Ufaransa.
Mashindano hayo yatafanyika katika maonyesho ya kwanza ya kitaifa ya Athari za Kiislamu.
Katika maonyesho hayo yatakayofanyika kwa mara ya kwanza katika mji wa Val d'Oise kutakuwepo pia vikao vya kujadili sira na maisha ya Mtume Muhammad (saw) na hotuba za wasomi na maulama wakubwa wa Ulaya na Mashariki ya Kati. Vitabu vya lugha mbalimbali pia vitaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Vilevile kutakuwepo meza za mijadala zitakazojadili uchumi wa Kiislamu, mafundisho ya kidini nchini Ufaransa, nafasi ya Nabii Issa Masiih (as) kwa Waislamu, njia za kuarifisha Uislamu kwa watoto wadogo na umuhimu wa kutambua itikadi za dini nyingine na taathira zake katika kuishi kwa amani.1001860


captcha