Ramin Mehmanparast amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari na kuongeza kwamba, aina yoyote ile ya ukosefu wa amani na usalama huko Afghanistan inaweza kuwa na taathira mbaya kwa usalama wa Iran.
Mehmanparast amekosoa utiwaji saini wa mkataba wa usalama kati ya Marekani na Afghanistan na kusema kwamba, chanzo kikuu cha ukosefu wa amani na utulivu Mashariki ya Kati hususan Afghanistan ni kuweko vikosi vya kigeni vikiwemo vya Marekani katika eneo hili.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameashiria zoezi la uchaguzi wa Bunge lililofanyika jana nchini Syria na kusema kuwa, uchaguzi huo ni hatua ya pili muhimu ya serikali ya Damascus katika njia ya mageuzi.
Kwingineko katika matamshi yake, Mehmanparast amesema kupewa hifadhi wanachama wa kundi la kigaidi la MKO katika nchi jirani ya Jamhuri ya Azerbaijan kutapokelewa kwa jibu kali la Iran. Mehmanparast amedokeza kuwa mpango huo ni katika njama za Wazayuni na Wamarekani.
1003094