Kwa mujibu wa tovuti ya echoruoukonline, taasisi ya Abul Hudaa imezindua mpango huo katika mjii mkuu Algiers.
Mpango huo pia unajumuisha maonyesho kuhusu aina 10 za qiraa ya Qu'ani Tukufu, qiraa bora za Qur'ani Tukufu na vilevile vikao maalumu kuhusu ufahamu wa tajwidi katika miji mbalimbali ya Algeria.
Mpango huo pia utakuwa na darsa za Qur'ani na historia ya Qur'ani.
Waandalizi wa mpango huo wamesema watatumia teknolojia za kisasa katika kutoa mafundisho ya tajwidi.
Pembizoni mwa mafundisho hayo kutakuwa na mpango wa mashindano ya qiraa miongoni mwa familia ili kutathmini ujuzi waliopata washiriki.
1002984