Mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu wa nchini Tunisia amewasilisha mashtaka mahakamani akitaka kutiwa nguvuni Sheikh Yusuf Qardhawi, mwanazuoni wa Qatar ambaye amefanya ziara nchini humo kwa tuhuma kuwa amechochea mifarakano kati ya Waislamu.
Ombi la mwanaharakati huyo ambaye pia ni wakili mashuhuri wa Tunisia limewasilishwa kwa mwendesha mashtaka wa nchi hiyo katika hali ambayo miezi kadhaa iliyopita serikali ya Imarati ilimtuhumu mwanazuoni huyo ambaye ni mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu, kuwa anachochea na kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo, na kutaka atiwe nguvuni kutokana na jambo hilo.
Wakili huyo amewataka viongozi wa Tunisia wamtie mbaroni Qaradhawi mara moja kutokana na uchochezi wake dhidi ya Waislamu na kuwataka wajihusishe na vitendo vya ghasia na fujo. Amewataka watawala wa nchi hiyo watekeleze hatua hiyo haraka iwezekanavyo na kumzuia mwanazuoni huyo kutoka nchini humo.
Katika miaka ya hivi karibuni Qardhawi amekuwa akitoa matamshi ya kichochezi na mara nyingine yanayogongana wazi na maslahi ya umma wa Kiislamu. 1003700