Akibainisha suala hilo, Qamar Alim, mkuu wa taasisi hiyo amesema kwamba kabla ya kuanza masomo hayo, wanazuoni na wafanyakazi wa taasisi za kidini walikutana kwa lengo la kutafuta mbinu bora zaidi za kutolewa masomo hayo.
Amefafanua umuhimu wa masomo hayo na kuongeza kuwa yatahusiana na namna ya kusoma Qur'ani Tukufu kwa mbinu tofauti na vilevile itikadi na sheria za Kiislamu. Masomo hayo yamepangwa kumalizika mwishoni mwa mapumziko ya msimu wa joto.
Mwishoni mwa mkutano huo, Jahangir mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa India amesisitiza udharura wa kufahamu vyema tauhidi ya Mwenyezi Mungu na misingi ya itikadi ya Kiislamu, pamoja na kujiepusha na mila zinazokwenda kinyume na misingi hiyo. 1002969