Hayo yamesemwa na mwanaharakati wa Kiislamu wa Nigeria Ibrahim Mussa, katika mahojiano yake ya IQNA. Amesema kwa kawaida mafundisho ya Qur'ani huanza katika kipindi cha umri wa miaka minne wakati mtoto anapoanza kuzungumza na kuelewa anayoambiwa na mwanzoni hufunzwa sura fupi fupi za Qur'ani Tukufu.
Ibrahim Mussa ameongeza kuwa katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria watoto wadogo hupelekwa kwa mwalimu wa Qur'ani baada ya kuhifadhi Qur'ani. Mussa ambaye ni mhariri wa gazeti la al Mizan anasema mbali na madrasa za kijadi, Qur'ani pia hufundishwa katika shule za Kiislamu.
Amesema kuwa katika shule hizo za Qur'ani hutayarishwa mashindano makali ambayo yanazidisha hamu za kujifunza na kupata elimu na mafundisho zaidi ya Qur'ani baina ya wanafunzi.
Amesema kuwa makarii wa Qur'ani nchini Nigeria hufuatilia kiraa ya wasomaji mashuhuri duniani kama Minshawi na wengineo na mara nyingi hutumia kaseti na sidi za sauti za makarii hao. 1002009