Kikao hicho kinadhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Nchi za Kiilamu ISESCO kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani Tukufu na kimepangwa kufanyika katika ukumbi wa Mfalme Fahd katika Jamhuri ya Chad. Zaidi ya wasomi, wataalamu na wawakilishi wa taasisi za hifdhi ya Qur'ani 50 kutoka nchi mbili hizo wamealikwa kushiriki kikao hicho na kubadilishana mawazo kuhusiana na nafasi ya mahafidh wa Qur'ani tukufu katika kuimarisha jamii za nchi za Kiafrika. Kuwashirikisha mahafidh katika masuala ya umma wa Kiislamu, kuongeza ujuzi wao kuhusiana na masuala ya mafunzo ya Kiislamu na kijamii, kuwashirikisha zaidi katika masuala ya kuimarisha jamii ya kimataifa, kubadilishana uzoefu na kuandaliwa mipango ya kuimarisha vituo vya Qur'ani ni malengo mengine ya kufanyika kikao hicho. 1004990