IQNA

Saudia kutoa dola bilioni 4 kwa ajili ya kumpa hifadhi Mubarak

12:12 - May 12, 2012
Habari ID: 2323700
Naibu mkuu wa chama cha Ikhwanul Muslim cha Misri amefichua kwamba Saudi Arabia imependekeza kutoa dola bilioni 4 kwa ajili ya kumpa hifadhi dikteta Husni Mubarak aliyengo'lewa madarakani hivi karibuni nchini Misri.
Kheirat as-Shatir naibu mkuu wa Ikhwanul Muslimin amefichua kwamba Saudia imetoa pendekezo hilo ili kumpokea na kumpa hifadhi dikteta huyo wa zamani wa Misri ambaye anazuiliwa jela nchini humo. As-Shatir amesema kuwa wananchi wa Misri ndio wanaopasa kuwa na neno la mwisho kuhusu kadhia hiyo kwa sababu utawala wa dikteta huyo ulipora na kuharibu mali ya umma wa taifa hilo. Amesema asilimia 40 ya wananchi wa Misri wanaishi chini ya mstari wa umasikini na kwamba chama cha Ikhwanul Muslimin kitafanya kila liwezekanalo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wa nchi hiyo. 1005106
captcha