IQNA

Wairani wapinga mpango wa Marekani wa kuunganisha Saudia-Bahrain

12:28 - May 19, 2012
Habari ID: 2328983
Wairani wameandamana kulalamikia mpango hatari wa Saudi Arabia wa kuiteka ardhi ya Bahrain na kuifanya kuwa milki yake. Aidha wamelaani vikali ukandamizaji dhidi ya wananchi wa Bahrain unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa.
Maandamano hayo yalifanyika baada ya sala ya Ijumaa mjini Tehran na miji mingine ya Iran ambapo washiriki wameutaja mpango huo kuwa uhaini kwa watu wa Bahrain.
Saudi Arabia inataka kuiteka ardhi ya Bahrain kwa madai kuwa ni katika mpango wa kuziunganisha nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.
Nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi zinazojumuisha Saudi Arabia, Kuwait, Bahrain, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu na Oman walikutana Jumatatu iliyopita mjini Riyadh kujadili mpango huo. Hatahivyo hawakuweza kufikia muafaka.
Wananchi wa Bahrain pia waliandamana baada ya sala ya Ijumaa kulaani kuiunganisha Bahrain na Saudi Arabia. Harakati ya al Wifaq imesisitiza kwamba mpango huo umezushwa kwa lengo la kuisambaratisha jamii ya Bahrain. Sambamba na radiamali hiyo ya harakati ya al Wifaq, wananchi wa Bahrain pia wamefanya maandamano katika miji mbali mbali ambapo mbali na kupinga mpango wa kuunganishwa nchi yao na Saudia wametoa nara na sha'ar pia dhidi ya utawala wa Aal Khalifa.
1010778
captcha