IQNA

11:00 - May 20, 2012
News ID: 2329687
Kozi ya Qur’ani Tukufu imekamilika Mei 17 katika Msikiti wa Imam Hussein AS katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA tawi la Dubai, sherehe za kufunga hafla hiyo zilifanyika kwa mnasaba wa siku za kukumbuka uzawa wa Bibi Fatima Zahra SA.
Hafla hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Qur’an na Etrat na ilifanyika baada ya sala ya Isha na kuhudhuriwa na wanafunzi wa taasisi hiyo pamoja na wazazi wao.
Ayatullah Madani alitoa hotuba katika hafla hiyo na kuwatunuku zawadi wanafunzi waliofuzu.
Aidha wanafunzi wa taasisi hiyo walihudhuria semina iliyofanyika msikitini hapo.
1010461
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: