IQNA

Bendera ya “Ali Aliyezaliwa Ndani ya Kaaba” kupandishwa juu ya Kuba ya Haram ya Imam Ali (AS)

15:44 - December 28, 2025
Habari ID: 3481728
IQNA – Uwanja wa Haram Tukufu ya Imam Ali (AS) mjini Najaf, Iraq, leo tarehe 28 Disemba 2025 umeshuhudia hafla ya kupandisha bendera maalum.

Hafla hii imefanyika kabla ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam wa Kwanza (AS).

Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ali (AS) imetangaza kuwa: “Kutoka chini ya kivuli cha haram tukufu ya Kiongozi wa Waumini (AS), kwa pumzi takatifu za Wilayah na kwa furaha ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Kiongozi wa Waumini Ali ibn Abi Talib (AS), bendera ya kuzaliwa itapandishwa.”

Taarifa hiyo imeongeza: “Kila mmoja amealikwa kushiriki katika hafla ya kupandisha bendera ya kuzaliwa kwa Kiongozi wa Waumini Ali ibn Abi Talib (AS) katika tukio hili lililobarikiwa.”

Astan imeandaa ratiba kamili ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Ali (AS) katika tarehe 13 Rajab (3 Januari 2026), ikihusisha idara zote na vitengo vyake, na itadumu kwa wiki moja.

Aidha, maandalizi yamefanywa kwa ajili ya kuwatumikia wafanyaziyar watakaotembelea haram ya Najaf kushiriki katika tukio hili.

Kwa heshima ya kumbukumbu hii, idara hiyo pia imepamba haram tukufu kwa maelfu ya maua yenye harufu nzuri.

3495875

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al kaaba imam ali najaf
captcha