
Sherehe hii iliandaliwa chini ya kauli mbiu “Gaza itastawi kwa Wanaohifadhi Qur’an”, kwa mujibu wa shirika la habari la Al-Boslah. Tukio hili lilifanyika mitaani mwa Kambi ya Al-Shati kwa shangwe na furaha kubwa.
Baada ya kumalizika kwa vita vya kikatili vilivyodumu kwa miaka miwili katika Ukanda wa Gaza, sherehe hii ilileta tena hisia za furaha, matumaini na utulivu katika mitaa ya kambi hiyo.
Hafla hii ilidhaminiwa na Taasisi ya Ayad Al-Khair pamoja na Taasisi ya Kihisani ya Kuwait Aaliyah. Washiriki walitembea kwa mpangilio mzuri katika njia za kambi, wakibeba nakala za Qur’an Tukufu, bendera ya Palestina na mabango, huku wakipiga Takbir na Tahlil, wakionesha ujumbe wa kusimama imara.
Wakazi wa kambi walijiunga kando ya njia kwa dua na hamasa, hali iliyobadilisha mitaa iliyoharibiwa na vita kuwa mahali pa amani na mshikamano kwa muda wa saa chache.
Ibtisam Abu Huwaydi, mmoja wa wanaohifadhi Qur’ani aliyekamilisha kuhifadhi Qur’ani yote wakati wa vita, alisema: “Kuendelea kuhifadhi Qur’ani chini ya mashambulizi ya mabomu haikuwa rahisi, lakini Qur’ani imenipa nguvu na utulivu katika nyakati ngumu zaidi.” Alisisitiza kuwa kushikamana na Qur’an ni njia ya kudumisha matumaini.
Aidha, Abu Huwaydi alieleza matumaini yake kwamba watoto wake wanne pia watahifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na akawahimiza vijana wa Gaza kushikamana na Qur’ani na kuitafakari, hususan katika hali ngumu za sasa.
Mushira Abu Watafah, mzazi wa mmoja wa wanaohifadhi, alibainisha kuwa watoto waliendelea kushiriki katika duru za kuhifadhi Qur’ani licha ya umasikini na mzingiro, akisema: “Sherehe hii imeinua ari ya watu na kuimarisha imani yao katika nafasi ya Qur’ani katika maisha ya mtu binafsi na jamii.”
Mwisho wa sherehe, wanaume na wanawake waliokamilisha kuhifadhi Qur’an walikabidhiwa vyeti vya shukrani na zawadi za heshima. Waandaaji walisisitiza kuwa mpango huu ni sehemu ya juhudi za watu kuhifadhi utambulisho wa kidini na maadili katika mazingira magumu ya Gaza.
Tarehe 8 Oktoba 2023, utawala wa Kizayuni Isral, ukiungwa mkono na Marekani, ulianzisha mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza yaliyodumu kwa miaka miwili na kusababisha shahada ya takriban Wapalestina 71,000, kujeruhiwa kwa zaidi ya watu 171,000, na uharibifu mkubwa ulioteketeza asilimia 90 ya miundombinu ya kiraia. Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi hicho, misikiti zaidi ya 835 iliharibiwa kabisa na zaidi ya misikiti 180 kuharibiwa kwa sehemu.
/3495861
Zenye maoni mengi zaidi