Katika Surah Al-Imran, watu wanahimizwa kukimbilia msamaha na Pepo isiyo na kikomo (Aya ya 133) isemayo: "Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu."
Baada ya kutaja baadhi ya sifa, ikiwemo Istighfar, Mwenyezi Mungu anasema: “Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao.” (Aya ya 136 ya Surah Al-Imran). Hii ina maana kwamba miongoni mwa masharti ya wale watakaotangulia kuingia Peponi ni Istighfar.
Katika aya za mwanzo za Surah hii, thawabu ya wachamungu katika Pepo imetajwa kwanza, kisha katika kueleza hali yao ya kidunia, Mwenyezi Mungu anasema: Wanao subiri, wanao sema kweli, na wat´iifu, na wanao toa sadaka, na wanao omba maghafira kabla ya alfajiri.” (Aya ya 17 ya Surah Al-Imran).

Katika Surah Adh-Dhariyat, Mwenyezi Mungu ametaja makazi ya wachamungu katika bustani na chemchemi za Pepo na kupokea zawadi kutoka kwa Mola: “Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.” (Aya ya 15-16).
Aya ya 15 inaanza kwa neno “kupokea” na kuishia kwa “Muhsinin” (wafanyao wema). Hii inaonyesha kuwa kupokea kheri katika Pepo ni matokeo ya kufanya wema na kuwatendea wengine wema hapa duniani. Kisha ikataja sifa mbili za kawaida: “Walikuwa wakilala kidogo tu usikui. *Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira." (Aya ya 17-18).
Muktadha wa vitenzi katika aya hizi unaonyesha mwendelezo. Aya hizi zinaonyesha kuwa kusimama usiku kwa sala na kuomba msamaha alfajiri ni ada ya kudumu ya watu watakaoingia Peponi. Pia zinaashiria kuwa asubuhi, miongoni mwa dhikr zote, Istighfar ina nafasi maalum na inachukuliwa kuwa kilele cha ibada.
/3495305
Zenye maoni mengi zaidi