Kwa mujibu wa tovuti ya Nun afisa huyo amesema kuwa ujumbe huo ulitumwa kwa idara inayosimamia eneo hilo takatifu la ziara na makundi ya magaidi wa Kiwahabi. Afisa huyo amesema kuwa ujumbe huo wa kushambuliwa Haram ya Bibi Rukia umetumwa kwa idara hiyo sambamba na kuongezeka mashambulio ya kigaidi ya Mawahabi dhidi ya Mashia mjini Damascus. Katika shambulio lao la hivi karibuni dhidi ya Mashia, Mawahabi wameshambulia na kumuua shahidi imamu wa Msikiti wa Bibi Rukia (as). Kwa mujibu wa ripoti hiyo hatua kali za kiusalama zimechukuliwa kwa ajili ya kuilinda Haram ya Bibi Rukia kutokana na mashambulio ya magaidi wa Kiwahabi. Kabla ya hapo magaidi hao walishambulia kwa risasi na kumuua shahidi Sayyid Nasir al-Alawi, hatibu na imamu wa swala ya jamaa wa Husseiniya ya Alawiya katika eneo la Zeinabiya katika mji wa Damascus. 1012115