IQNA

Waislamu Uholanzi wanabaguliwa

9:40 - May 22, 2012
Habari ID: 2331209
Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha ubaguzi mkubwa dhidi ya jamii ya Waislamu Uholanzi.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA barani Ulaya, uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na shirika la Maurice De Hond unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya Waislamu wahajiri nchini Uholanzi wanalalamika kuwa wanabaguliwa kwa msingi wa dini yao.
Asilimia 58 ya waliohojiwa walisema wanaamini kuwa muamala wa serikali ya Uholanzi na Waislamu ni wa kibaguzi ikilinganishwa na wahajiri wanaofuata itikadi zinginezo.
Asiliamia 2 ya waliohojiwa walisema hawajui iwapo ubaguzi upo huku asilimia 40 wakidai kuwa serikali ya Uholanzi haiwadhulumu Waislamu.
Uchunguzi huo wa maoni uliwahusisha Waislamu 700 kwa njia ya ana kwa ana na simu kuanzia Aprili 22-24 mwaka 2012 na kuchapishwa Mei 4.
Jamii ya Waislamu Uholanzi aghalabu inajumuisha wahajiri kutoka Morocco na Uturuki ambao wameingia nchini humo kupitia njia za kisheria. Waislamu Uholani hawashiriki kwa wingi katika uchaguzi kutokana na muamala mbovu wa utawala wa Uholanzi. Ikumbukwe kuwa shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limechapisha ripoti hivi karibuni iliyokosoa Uholanzi kwa kuwabagua Waislamu hasa katika masuala ya elimu na ajira. Ripoti hiyo pia ilikosoa tawala za Ubelgiji, Ufaransa, Uhispania na Uswishi kwa kuwabagua na kuwadhulumu Waislamu.
1012952
captcha