Kati ya mawaziri 34 katika serikali ya Hollande mawaziri Waislamu ni Najat Vallaud-Belkacem, Yamina Benguigui na Kader Arif.
Bi. Belkacem,34, mwenye asili ya Morocco ameteuliwa kuwa waziri wa haki za wanawake, nafasi ambayo haikuwepo katika serikali iliyopita. Aidha Belkacem ambaye alikuwa msemaji wa kampeni ya urais ya Hollande ameteuliwa pia kuwa msemaji wa serikali.
Mwislamu mwingine waziri ni Bi. Yamina Benguigui waziri mdogo wa Wafaransa waishio nje ya nchi. Ana asili ya Algeria ni ni mtengeneza filamu. Mwislamu wa tatu katika baraza la mawaziri Ufaransa ni Bw. Kader Arif ambaye anashikilia nafasi ya waziri mdogo wa masuala ya maveterani wa kivita. Arif amekuwa akiulaumu utawala haramu wa Israel kwa kusababisha matatizo katika sera za kigeni za Ufaransa.
Waislamu Ufaransa katika uchaguzi wa rais wa hivi karibuni waliongoza kampeni iliyopelekea kuangusha Nickolas Sarkozy ambaye analaumiwa kwa kueneza sera za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
1013742