IQNA

Al Qaeda na wenye misimamo wanazuia Mwamko wa Kiislamu

13:13 - May 22, 2012
Habari ID: 2331605
Misimamo ya kufurutu mipaka inapatikana katika kila dini na utaifa wenye misingi wa ubaguzi nao pia unazidi kuibuka kama ilivyoshuhudiwa huko Norway mwaka jana. Lakini kwa nini Waislamu wawe na hofu kuhusu kila kitengo cha ugaidi na kwa nini Waislamu wanalaumiwa baada ya kila kitendo cha ugaidi.
Ni nani anayetabasamu kila wakati bomu linapolipuka Karachi, Peshawar, New Delhi, Kabul, Baghdad au Madrid kwa jina la dini au dhehebu? Bila shaka ni wale wote wanaoutazama ulimwengu kwa mtazamo wa kufurutu mipaka. Ingawa Wamagharibi wanadai kuwa Ukristo wenye misimamo mikali hauko tena na kwamba eti ni Waislamu tu wenye kutenda ugaidi, hilo si kweli.
Ukweli ni kuwa misimamo ya kufurutu mipaka inapatikana miongoni mwa wafuasi wa kila dini.
Kuua watu wasio na hatia ni jambo ambalo haliwafurahishi Waislamu, na kama wengine wote, wanalaani vitendo hivyo vya kishenzi.
Wale ambao wanaunga vitendo vya wafuasi wa Bin Laden, Al Qaeda au makundi mengine yenye misimamo ya kufurutu mipaka kama Taliban, sawa na Wakristo wenye misimamo mikali, ni sehemu ndogo tu ya Waislamu duniani na hawakaribishwi katika jamii za Waislamu.
Leo, kwa ustawi wa sayansi na sayansi, teknolojia na mitandao ya mawasiliano, kila mtu anaweza kupata vyanzo vikuu vya Uislamu (Qur’ani Tukufu na Seerah ya Mtume SAW) ili kuujua Uislamu. Maamurisho ya dini tukufu ya Kiislamu yamejengeka katika msingi wa hekima na kila ambacho kinakiuka hekima hakina chanzo cha Tauhidi.
Al Qaeda na watu wengine wenye misimamo mikali ambao huendesha oparesheni zao kwa jina la Uislamu wanazuia wimbi la Mwamko wa Kiislamu, lakini kwa bahati nzuri Waislamu halisi wako macho na daima wanafuata misimamo ya kati.
Waislamu wa kweli wanataka mshikamano na umoja wenye kuleta pamoja mataifa ili kuhuisha ustaarabu wa Kiislamu kwa msingi wa maadili bora.
Ni jukumu la vijana wote katika nchi za Kiislamu kutambua na kulaani watu wenye misimamo mikali inayofurutu ada na kupinga misimamo hiyo inayokiuka mafundisho ya Kiislamu.
Na: Hadi A’alami Fariman
1012892

captcha